Stars maboresho kuivaa Rwanda

465

Kikosi cha Taifa Stars Maboresho kitacheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya Rwanda itakayofanyika Januari 22 mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mechi hiyo ni sehemu ya programu ya Kocha Mart Nooij kuiandaa timu hiyo kwa ajili ya mechi za mchujo michuano ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN).

Mechi za mchujo za michuano hiyo ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Rwanda zinaanza Mei mwaka huu.

Kocha Nooij anatarajia wakati wowote kutangaza kikosi cha timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager ambacho kitakusanyika Januari 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam, na siku moja baadaye kwenda jijini Mwanza.

Yaya Toure mwanasoka bora

03

kiungo wa timu ya Manchester City Yaya Toure amekuwa mchezaji wa kwanza kutajwa na shirikisho la soka barani Afrika kuwa mchezaji bora wa mwaka kwa mwaka wanne mfululizo.

Toure ana umri wa miaka 31,aliteuliwa baada ya kucheza kwa kujitoa na kuleta ushindi katika Premier League na League Cup, na pia alijitoa kuisaidia Ivory Coast kuingia katika kombe la mataifa ya Africa yatakayo fanyika baadaye mwaka huu.

Toure amewapiku mshambuliaji kutoka Gabon, Pierre Emerick Aubameyang na golikipa mnigeria Vicent Enyeama.Toure pia alikwaa tuzo ya FIfa ya Ballon D’Or mwezi wa kumi mwaka wa jana..

Yanga yaaga kombe la Mapinduzi

Yanga imeng’oka katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa bao 1-0 na JKU.

JKU inayomilikiwa na Jeshi la Zanzibar imefanikiwa kuing’oa Yanga katika mechi kali na ya kuvutia kwenye Uwanja wa Amaan, huko Zanzibar.

Muuaji wa Yanga alikuwa Amour Mohammed ambaye alifunga bao hilo adhimu kabisa katika dakika ya 72 na kupeleka simanzi Jangwani,kitendo kilichoivuruga Yanga wasionane na kushindwa kusawazisha ,ingawa watoto hao wa Jangwani watajilaumu wenyewe kwa kupoteza nafasi kadhaa za kufumania nyavu bila mafanikio katika kipindi cha kwanza.

Kutokana na ushindi huo, sasa JKU itacheza nusu fainali dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo iliing’oa Azam FC .66

UN yakemea mashambulizi dhidi ya Albino

Umoja wa Mataifa umekemea wimbi la mashambulizi dhidi ya Watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino, baada ya tukio la kutekwa kwa mtoto wa miaka minne mjini Mwanza, kaskazini magharibi mwa Tanzania.

Mwakilishi wa UN nchini humo Alvaro Rodriguez ameitaka Serikali ya Tanzania kuzidisha juhudi za kupambana na vitendo vya unyanyapaa dhidi ya albino.

Akiwa katika ziara kanda ya ziwa, Mjumbe huyo wa UN amekemea kutekwa kwa binti mdogo na kutoa wito kwa serikali kufanya kila iwezalo kumuokoa na kumkutanisha na Familia yake.

Mtoto Pendo Emmanuel alitekwa akiwa nyumbani kwake Kijiji cha Ndami baada ya Watu kadhaa wakiwa na mapanga kuvamia makazi yao tarehe 27 mwezi Disemba mwaka jana.Polisi wamesema Watu 15 akiwemo Baba yake wamekamatwa wakihusishwa na tukio la kutekwa kwa mtoto huyo.455

Riadha:Sheria dhidi ya dawa zatolewa

Shirika la riadha nchini AK limetoa orodha ya sheria za kukabiliana na wanaraidha wanaoutumia dawa za kusisimua misuli huku kukiwa na ongezeko la ripoti kuhusu wanariadha wa Kenya ambao wamefeli ukaguzi wa dawa hizo.

Sheria hizo zimetolewa siku tatu kabla ya mshindi mara tatu wa mashindano ya Boston Marathon Rita Cheptoo kufika mbele ya tume ya kukabiliana na dawa hizo katika shirika la riadha la Kenya AK ambapo kesi yake itasikizwa.

Cheptoo wa Kenya alifanikiwa kulitetea taji lake la Boston Marathon alipoweka rekodi ya masaa 2 dakika 18 na sekunde 57.141216135401_kenya_athletes_640x360_b_nocredit