Yanga yaendea kombe la shirikisho Zambia

Na Mwandishi Wetu
KLABU ya soka ya Yanga inatarajia kuondoka jijini kuelekea nchini Zambia kushiriki mashindano ya kirafiki kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya kombe la Shirikisho.
Yanga inatarajia kuiwakilisha nchi katika michuano hiyo inayozikutanisha timu zilizoshika nafasi ya pili katika michuano ya ligi kuu ya nchii mwao.
Akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu katibu mkuu wa Yanga DR Jonas Tiboroha alisema michuano hiyo imepanga kuanza Februari 28 hadi Machi 4 nchini Zambia.
Tiboroha alisema timu yao inatarajia kuondoka jijini Dar es Salaam baada ya mchezo wao wa hatua ya 12 ya ligi kuu ya bara,inayoendelea kwa baadhi ya timu ambazo hazijaenda katika michuano ya kombe la Mapinduzi.
Aliongeza kuwa wamepata mwaliko wa barua kutoka kwa wenyeji wao timu ya Zesco ya Zambia ambapo wanasema wanatarajia kukutana na timu ya El Hirary ya Sudan,Msumbuji, Malawi, Afika Kusini na Rwanda ambazo nazo zimepata mwaliko wa mashindano hayo.
Alisema kutokana na mwaliko huo wamekubali kushiriki katika mashindano hayo, ambayo wanaimani yatawasaidia katika maandalizi ya michuano ya kombe la Shirikisho linaloshirikisha timu zilizomaliza ligi zikiwa katika nafasi ya pili.
“Tumefrahi kupata mwaliko huu, kwa sababu tunakwenda kukutana na timu kubwa ambazo zitatupa mazoezi ya kutosha kabla ya kushiriki kombe la Shirikisho,”alisema Tiboroha.
Alisema kikosi chao kiko vizuri kwa sasa kutokana na mazoezi wanayopata chini ya makocha Hans Van Pluijm na Boniface Mkwasa ambao wameanza kombe la Mpainduzi kwa kuichapa timu ya Jang’ombe mabao 4-0.
Akizungumzia kwa upande wa kikosi chao kwa ujumla alisema kwa sasa kipo vizuri kutokana na kucheza kwa kasi huku wakionana pale wanapokuwa uwanjani kucheza na timu pinzani.
“Timu kwa sasa inatia moyo unapoiona inacheza uwanjani, wachezaji wanajituma sana,”alisema Tiboroha.
Katika hali nyingine Tiboroha alisema wanatarajia kuiandikia barua Shirikisho la soka nchini TFF ya kuomba kuahirishwa kwa mchezo wao wa hatua ya 13, ili waende katika michuano hiyo ya kujipima nguvu nchini Zambia.

Mwisho.

yanga fc

yanga fc

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s