Mtibwa yavutwa shati kombe la Mapinduzi

Mwandishi wetu
PAMOJA na kutangulia kufunga kwa goli la kipindi cha kwanza lililofungwa na mshambuliaji Mussa Hassan ‘Mgosi’, kikosi cha Mtibwa jana kilishindwa kulinda goli hilo na kujikuta kikilazimishwa sare ya kufungana goli 1-1 na JKU katika michuano inayoendea mjini hapa ya Kombe la Mapinduzi.
Mtibwa iliingia uwanjani kwenye mchezo wa jana kwenye uwanja Amaan mjini hapa huku ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa goli 1-0 walioupata mbele ya Simba kwenye mchezo wa ufunguzi.
Iliwachukua Mtibwa dakika 20 kupata goli kupitia kwa Mgosi akiitendea haki klosi iliyopenyezwa na beki mkongwe wa timu hiyo, Said Mkopi.
Pamoja na kushambuliana kwa zamu, goli hilo lilidumu kwa kipindi chote cha kwanza na timu kwenda mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Mtibwa walifanikiwa kupata penati lakini Mgosi alishindwa kuukwamisha mpira wavuni na penati yake kupaa juu.
Penati hiyo ilitolewa baada ya beki wa kati wa JKU, Suleiman Omari kuunawa mpira akiwa kwenye eneo la hatari.
Dakika ya 60, Kocha wa Mtibwa, Meck Maxime alifanya mabadiliko kwa kumtoa mfungaji wa goli, Mgosi na nafasi yake kuchukuliwa na winga, Vicent Barnabas, hata hivyo mabadiliko hayo hayukuonekana kuisaidia sana Mtibwa ambapo katika dakika ya 72, Amour Omar aliisawazishia JKU baada ya kuunganisha kiufundi klosi safi iliyopigwa na Mohamed Abdallah.
Hilo ni goli la pili katika michuano hiyo kwa Omar ambaye pia ni kinara wa magoli katika ligi kuu ya Zanzibar akiwa na magoli nane.
Kwa matokeo hayo, Mtibwa na JKU zote zimefikisha pointi nne kwenye kundi lao lenye pia timu za Simba na Mafunzo ambazo zote zilipoteza michezo yao ya kwanza kwenye kundi lao.
Simba ililala kwa goli 1-0 mbele ya Mtibwa huku Mafunzo ikikumbana na kipigo cha magoli 2-0 kutoka kwa JKU.
JKU na Simba zilitegemewa kucheza jana saa 11 jioni.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s