Hatubweteki kwa ushindi’

Na Mwandishi Wetu
KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Mtibwa Sugar Mecky Mexime amesema timu yake haitabweteka katika michuano hiyo baada ya kuifunga Simba kwa bao 1-0, katika mechi ya ufunguzi ya michuano ya kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar.

Mtibwa juzi ilianza vema mashindano hayo, baada ya kuwatoa nishai Simba ya kuwafunga bao 1-0, katika mashindano hayo chini ya kocha Msebia na kocha msaidizi Seleman Matola.

Akizungumza kwa njia ya simu na NIPASHE Mexime alisema kikosi chake hakiwezi kubweteka na ushindi huo kutokana na kwamba bado wanakabiliwa na na mechi ngumu katika mashindano hayo.

“Timu yangu haiwezi kubweteka na ushindi dhidi ya Simba, bado tutaendelea kufanya mazoezi ya kutosha ili kuendelea kufanya vizuri katika mechi zijazo za michuano hiyo,”alisema Mexime.

Alisema ushindi wa dhidi ya Simba umewapa changamoto kubwa ya kuendelea kufanya mazoezi ili kuhakikisha wanashinda katika mechi nyingine za kundi lao ambazo wanaimani watasonga mbele na kufika hatua ya fainali ya mashindano hayo.

Akizungumzia kwa upande wa michuano hiyo kwa ujumla alisema wanaitumia kama moja ya mazoezi ya kujiandaa na hatua ya tisa ya ligi kuu ya bara iliosimama kwa muda ili kupisha michuano ya kombe la Mapinduzi.

Alisema mara baada ya mashindano hayo anaimani kikosi chake kitakuwa kimeiva kwa ajili ya kukutana na Simba katika michuano ya ligi kuu ya bara hatua ya tisa,iliosimama kwa ajili ya kupisha kombe la mapinduzi.

Alisema timu yake msimu huu imejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano ya ligi kuu ili kuhakikisha anamaliza ligi huku wakiwa katika nafasi nzuri ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa ya soka.

Katika mashindano hayo Tanzania bara inawakilishwa na timu za Yanga, Simba, Azam FC na Mtubwa Sugar ambazo zote zipo visiwani humo kwa ajili ya kushiriki katika mashindano hayo.mtibwa

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s