Muuaji aaminiye kisu chake kitapata makali zaidi Real

Karim Benzema wa Real Madrid amejinasua kutoka kivuli cha Cristiano Ronaldo baada ya kiwango kizuri cha timu yake kuiacha ikikaa kileleni mwa msimamo wa La Liga na anaamini ataonyesha kiwango chake bora zaidi katika siku za usoni.
Mwezi mmoja tu uliopita Benzema alikuwa katika shinikizo kubwa kwani alikuwa amefunga magoli mawili tu katika mechi tisa lakini baada ya kiwango chake kuongezeka katika siku za karibuni amepokewa kwa mapenzi makubwa Bernabeu.
Mfaransa huyo alifunga bao pekee katika mechi ya mwishoni ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya ushindi dhidi ya Liverpool lakini hasifiwi kwa magoli bali kujituma kwake kwa faida ya wachezaji wengine kwenye mashambulizi.
Real inaongoza La Liga ikiwa na pointi 27 kutokana na mechi 10, ikifunga magoli 42, pointi mbili juu ya Barcelona. Benzema ameshirikiana vizuri na wenza wake katika ushambuliaji na hasa Ronaldo ambaye ana magoli 18.
“Sijui kama huu ndiyo uwezo wangu wa mwisho lakini najisikia vizuri, najituma, tunapata matokeo mazuri na nataka kuendelea hivi,” Benzema aliliambia gazeti la Marca.
“Nina miaka 26 na nadhani kipindi kizuri zaidi cha uchezaji wangu bado kipo mbele yangu. Watu wamekuwa wakiniambia kuwa unapofikisha umri wa miaka 26 au 27 na kuendelea ndiyo mchezaji anakuwa ameiva vizuri na nataraji ndivyo itakavyokuwa kwangu.
“Nitaendelea kucheza kwa bidii. Kwangu suala si tu kufunga kufunga magoli, ni dhana pana zaidi ya kuhusika katika mchezo na kutengeneza nafasi za kufunga — mara nyingine zinakuwa magoli na mara nyingine mashuti yanatoka nje.
“Nafurahia kucheza soka na kama naweza kuwasaidia wachezaji wenzangu kufunga basi inatosha. Huwa najaribu kumpa pasi Cristiano kwa sababu nataka afunge.
“Nina wasaa mzuri kwa sasa na timu pia. Tuna kikosi kabambe na ushahidi ni kwamba wachezaji wanaotokea benchini wanaweza kuleta mabadiliko na hilo ni la msingi katika timu.
“Ni muhimu kuwa na uelewano mzuri baina ya wachezaji, sisi ni timu na tunahitaji kusaidiana.”
Benzema anashukuru mno kwa sapoti anayopata kutoka kwa kocha Carlo Ancelotti ambaye alimuamini hata katika kipindi ambapo mpira ulikuwa umemkataa.
“Carlo siku zote amenikingia kifua kama ilivyo kwa rais. Miluzi ilitokana na watu kutegemea makubwa kutoka kwangu,” anasema. “Sijui kama nitazomewa tena  Karim_Benzema_Euro_2012_vs_Sweden_01uwanjani lakini ni sehemu ya soka.”

Karim_Benzema_Euro_2012_vs_Sweden_01

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s